Pamoko LGBTQ Mzuka
Angalia Video hii 👇 Mtunzi: CASEI KIALLE Facebook: PAMOKO Twitter: PAMOKO Instagram: PAMOKO YouTube: PAMOKO Jiunge Telegram Group FULL MZUKA: Ni jumamosi tulivu, hali ya hewa kibaridi kutokana na mvua ambayo ilikua ikinyesha tangu asubuhi. Mida hio ya saa tisa nilikua najiandaa kwenda kwenye party ya birthday ya best yangu Meddy. Kwenye saa kumi na moja kasorobo nilikua nabisha hodi kwa Meddy. “Hey Casey karibu!” alinikaribisha kwa bashasha Meddy. Baada ya kujuliana hali akaniongoza kwenda ndani. Alikua anaishi kwenye appartment moja hapo kinondoni. Ilikua ni kama nyumba ya nje, maana kuna nyumba kubwa ambayo ndio alikua anaishi mwenye nyumba, halafu ndio kuna hio ya nyuma. Ilikua ni kubwa na ina eneo la kutosha room mbili moja self-containing nyingine ya kawaida, kuna afu la wageni na choo chao sehemu ya kupikia na kula zimeungana kiaina ila sebule ilika pana na kutosha kuparty hata watu 10. Pale sebuleni palikua na watu watatu tayari hivyo mie nikawa wane na Med