Posts

Showing posts with the label karantini

Pamoko LGBTQ Karantin

Image
        Angalia Video hii 👇 Mtunzi: CASEI KIALLE Facebook: PAMOKO Twitter: PAMOKO Instagram: PAMOKO YouTube: PAMOKO K A R A N T I N I Habari ya mjini ilikua ni korona tu. Kila kona korona korona korona! Basi kama mamlaka zimesema tujifungie sasa nani atabisha! Kitu cha kushukuru ofisi niliyokua mafanya kazi inaruhusu hata kufanyia kazi nyumbani ilimradi uwe na laptop na internet. Basi nina wiki sasa niko home napiga kazi kama kawaida ila ndio hivyo tena bored sana maana hakuna kujichanganya wala niniNinapokaa ni apartment nimepangiwa na ofisi yangu. Ni jengo la ghorofa tano. Kwa jinsi hali inavyoonesha tuko wengi humu ambao hatuendi kazini kama mimi. Ni jumatano leo nimewahi kuamka mapema kuna kazi nilitakiwaniifanye na kuituma kabla ya saa tatu asubuhi, na niliikimbiza kweli ikakamilika. Mpaka saa tano nilikua nacheza game na kutazama movies tu. Mara nikasikia mlango wangu unagongwa! Nikajiinua kivivu kwenda kuangalia ni nani… “Jirani za asubuhi…” alikua ni jamaa ambae tu